Ijumaa 3 Julai 2026 - 00:06
“Makubaliano ya Washington” ni hati ya kujisalimisha inayowajibisha kuondolewa madarakani utawala

Hawza/ Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu nchini Lebanon umesisitiza kwamba: “Makubaliano ya Washington” yaliyotiwa saini kati ya utawala wa Lebanon na utawala vamizi wa Israel ni ukiukaji wa wazi wa Katiba ya Lebanon.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu nchini Lebanon, ukielezea kwamba “Makubaliano ya Washington” yaliyotiwa saini kati ya utawala wa Lebanon na utawala vamizi wa Israel ni ukiukaji wa wazi wa Katiba ya Lebanon, umesisitiza kuwa makubaliano hayo ni “hati ya kujisalimisha” ambayo imewapa wavamizi haki ya kubaki katika ardhi ya Lebanon na kuendelea kuikalia kwa mabavu.

Mkusanyiko huo umeeleza katika taarifa yake kwamba; kuingia kwa utawala katika makubaliano na adui kwa lengo la kuuangamiza muqawama (harakati za mapambano ya upinzani), ni kitendo cha usaliti kinachostahiki kuondolewa kwa utawala huo kupitia mifumo na taratibu za kikatiba.

Aidha, Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu umesisitiza kujitolea kwake kikamilifu katika mchakato wa mazungumzo ya Islamabad, na umewaomba viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuendelea kusisitiza utekelezaji na kuzingatiwa kwa kifungu cha kwanza cha hati ya maelewano kwa ajili ya kulinda misingi na kanuni za pamoja.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha